Prof. makame mbarawa aeleza sababu za Treni ya Sgr kutokwenda kasi ya Kilometa 160 kwa Saa leo

Tunayafanya uhakiki wa vichwa vya Treni kubeba mzigo kama ilivyokusudiwa

Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akizungumzia majaribio ya Awamu ya Pili ya Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, leo Machi 18, 2024 amesisitiza sababu za Treni hiyo kutokwenda kasi ya Kilometa 160 kwa Saa ni kutokana na kuwa katika majaribio

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) amesema “Tunayafanya uhakiki wa vichwa vya Treni kubeba mzigo kama ilivyokusudiwa, ndio maana majaribio ya awali ilikuwa mabehewa Matano, sasa hivi yamekuwa 14. Hadi Aprili 2024 tutakuwa tumefanya majaribio ya kwenda Dodoma.”

Share: