Pemba: rais dk.mwinyi ameifungua shule ya ghorofa ya sekondari kiwani iliyopo wilaya ya mkoani

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa kuwa vinara wa kutekeleza vizuri Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipofungua Shule ya ghorofa ya Sekondari Kiwani iliyopo Wilaya ya Mkoani , Mkoa wa Kusini Pemba ikiwa ni shamrashamra za Miaka ya 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.


Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuweka kipaumbele katika Sekta ya Elimu ambapo Rais Dk.Mwinyi amevipongeza Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuendelea kudumisha amani na utulivu nchini.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema Muungano ni muhimu kwa mustakabali wa maendeleo , amewataka Wananchi kuhakikisha wanaendelea kudumisha Muungano.

Share: