Naibu waziri kapinga afanya mazungumzo na watendaji wa kampuni ya mufindi paper mill

Naibu Waziri wa Nishati, ameipongeza kampuni hiyo kwa uwekezaji huo na kueleza kuwa Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano kadri itakavyowezekana kwani nia ya Serikali ni kufanya kazi pamoja na Sekta Binafsi katika nyanja mbalimbali ikiwemo umeme.

Kuhusu maombi mbalimbali yaliyowasilishwa na kampuni hiyo, Naibu Waziri ameelekeza wataalam kutoka TANESCO kushirikiana na Wataalam kutoka kampuni hiyo ili kuona namna bora ambayo Serikali kupitia TANESCO inaweza kutekeleza maombi hayo.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Nishati amefanya mazungumzo na watendaji kutoka Kampuni ya Songas wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Anael Samuel ambaye alieleza nia yao ya kujitambulisha kwa Naibu Waziri pamoja na kumweleza taarifa za sasa kuhusu uendeshaji wa kampuni hiyo inayozalisha umeme wa Megawati 190 na kuingiza katika gridi ya Taifa.

Share: