
Unadhani nini kifanyike ili kupunguza msongamano kwenye vituo na Usafiri wa mabasi yaendayo kwa haraka maarufu kama Mwendokasi..?
Ndani ya jiji la madaha liliosheheni idadi kubwa ya watu ,wenye shuguli mbali mbali. Kumekuwa na msongamano mkubwa wa watu kwenye vituo vya usafiri hususani vituo vya ma basi ya endayo kasi maarufu kama mwendokasi hususani hizi siku za karibuni.
Wakala wa mabasi ya endayo kasi (Dart) ndio wenye dhamna ya mabasi na huduma hio ya usafari,hawaja toa tamko lolote kuhusu changamoto ama sababu za ongezeko la msongamano wa watu kwenye vituo vya mabasi hasa ya mwendo kasi ambayo yameonekana kushindwa kutoa huduma inayokizi wasafiri wa jiji la Dar es salaam hususani barabara ya morogoro ,baada ya watu wengi kurundikana kwenye vituo wakisubiri mabasi kwa muda mrefu huku mabasi mengi ya kionekana kuharibika njiani.
Ungana nasi kwenye mitandai yetu ya kujami @stbongotv instagram,facebook,youtobe uweze kutoa maoni yako.
Ungana nasi kupitia kisumbuzi @startimestz CH 161 (antena) CH 401 (Dish) pamoja na kwenye YouTube channel yetu ya #STBongoTV Kwa Taarifa zaidi.