Mohammed dewji (mo) ametajwa kuwa tajiri namba 12 barani afrika

Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania na Rais wa heshima wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo) ametajwa na Jarida la Forbes kuwa tajiri namba 12 barani Afrika na bilionea kijana zaidi kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo.

Kwa mujibu wa jarida hilo mashuhuri ambalo hufuatilia ukwasi wa watu,ndani ya kipindi cha miaka miwili iliyopita Mo amepanda kiutajiri barani Afrika kutoka nafasi ya 15 hadi 12. Mbali na kupanda kiutajiri ukwasi wamfanyabiashara huyo anayemiliki Kampuni ya Mohammed Enterprises Ltd (METL), umepanda kutoka Dola za Marekani 1.5 bilioni (Sh3.77 trilioni) mwaka uliopita hadi Dola 1.8 bilioni(Sh4.52 trilioni) jambo linalomfanya kuwa tajiri namba moja ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa kwa ujumla ukwasi wa mabilionea 20 wanaoongoza Afrika uliongezeka kwa Dola 900 milioni (Sh2.26 trilioni) nakufika Dola Sh82.4 bilioni (Sh207.23 trilioni) mwaka 2024.

Upimaji wa ukwasi wa watu uliofanywa na Forbes uliangalia gharama halisi kwenye masoko ya mitaji na viwango vya kubadilishia fedha vilivyopo sokoni hadi Januari 8, 2024.

Share: