Mkuu wa mkoa wa dar es salaam chalamila amewahimiza wafanyabiashara, wafanyakazi na wananchi kulipa kodi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Chalamila amewahimiza Wafanyabiashara, wafanyakazi na Wananchi kwa ujumla kujitoa katika kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi kama sehemu ya kuchangia maendeleo na ustawi wa Taifa.

Chalamila ameyasema hayo jijini Dar es Salaam kwenye tukio la uzinduzi maalum ambapo amesema: "Naishukuru Wizara ya fedha kwa kuja na michakato inayowaelimisha watu kuhusiana na kodi na hasa kwa kuanzisha ofisi ya kuratibu shughuli hizo.

"Tukumbuke kua Taifa lolote duniani linategemea kodi kama chanzo cha mapato ya kujiendesha kwenye shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa huduma za jamii, hivyo hili sio jambo la hiyari, bali ni lazima.

"Kwa mantiki hiyo Wananchi ni lazima tujitoe kulipa kodi kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya Taifa."

Share: