Sambamba na kutembelea miradi hiyo ya maendeleo , Mhe. Senyamule pia amefanya Mkutano wa hadhara kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kijiji cha Ng’ambaku kilichopo katika Tarafa ya Mpwayungu Kata ya Ng’ambaku.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amefanya ziara ya kikazi kukagua Miradi ya shule ya Sekondari Ndogowe na Skimu ya umwagiliaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino tarehe 09 Januari 2024.
Katika ziara hiyo, Mhe. Senyamule amekagua Mradi wa Shule ya Ndogowe kupitia fedha za SEQUIP ambapo shule hiyo ilipokea kiasi cha shilingi Bilioni 544 kwa ajili ya Ujenzi wa madarasa 08, maabara 03, Jengo la utawala, Maktaba, Chumba cha TEHAMA, vyoo vya wanafunzi matundu 08 na Mradi wa Ujenzi wa Skimu ya umwagiliaji mashamba ya pamoja Ndogowe katika Kata ya Mlazo.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ilipokea jumla ya Shilingi Bilioni 21 ambapo imeingia Mkataba na Mkandarasi M/S.GNMS CONTRACTORS CO LIMITED kwa ujenzi wa skimu hiyo ya umwagiliaji.