Mkuu wa mkoa Albert chalamila amewakaribisha wakazi wa jiji la dar es salaam kwenye mapokezi ya ndege mpya boeing b737-9max

Mkuu wa mkoa wa Dar Es salaam Albert Chalamila amewakaribisha wakazi wa jiji la Dar Es salaam kwenye mapokezi ya ndege mpya ya BOEING B737-9MAX inayotarajia kuwasili kesho jumanne katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere.

Ndege hiyo yenye uwezo wa kuchukua abiria 181 itafika nchini ikitokea nchini Marekani ilipokuwa inatengenezwa.

Mgeni wa heshima atakayeongeza mapokezi ya ndege hiyo ni Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa akisindikizwa na baadhi ya mawaziri, wabunge na mabalozi mbalimbali.

Chalamila amewaambia wanahabari kuwa ujio wa ndege hiyo ni muendelezo wa jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha usafiri wa anga nchini.

Share: