Baada ya ziara hiyo Mhe. Kapinga alipata fursa ya kuzungumza na Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala huo Pamoja na Menejimenti ambapo Pamoja na mambo mengine ameulekeza wakala huo kueleza Umma majukumu wanayofanya katika kuwa hudumia watanzania.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga amekagua Maendeleo ya Ujenzi wa Miundombinu ya Kupimia Mafuta yanayoingia na kutoka nchini Pamoja na Ujenzi wa Mapipa mapya ya Kuhifadhi Mafuta Bandarini.
Mhe. Kapinga amefanya ziara hiyo ikiwa ni kufuatilia maelekezo ya Mhe. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati aliyoyatoa mwishoni mwa Mwezi Oktoba, 2023 alipotembelea Wakala huo na kuagiza kuwa Ujenzi wa Miundombinu Mipya ya kupimia Mafuta yanayoingia na kutoka nchini (Flow Meter) ikamilike kwa wakati na isiathiri utendaji kazi.
Flow Meter inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 na Mapipa hayo mapya yanamilikiwa na Serikali kwa Asilima 50 kupitia Kampuni yake ya Uhifadhi wa Mafuta TIPER Pamoja na Kampuni ya Orxy kwa Asilima 50 na yana uwezo wa kuhifadhi Lita za Ujazo Milioni 60.
Mara baada yakuona maendeleo ya Ujenzi huo, Mhe. Kapinga amesema kuwa Ujenzi wa miundombinu hiyo unaendelea vizuri na utakamilika kwa wakati kama ilivyoelekezwa.
Amesema kukamilika kwa Ujenzi wa Mapipa hayo mapya kutaongeza ufanisi wa kuhifadhi mafuta mengi zaidi tofauti na ilivyo sasa na kwa upande wa Flow Meter kutapunguza foleni za Meli za Mafuta Bandarini.
Baada ya ziara hiyo Mhe. Kapinga alipata fursa ya kuzungumza na Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala huo Pamoja na Menejimenti ambapo Pamoja na mambo mengine ameulekeza wakala huo kueleza Umma majukumu wanayofanya katika kuwa hudumia watanzania.