Mhe. dkt. tulia ackson amefungua maadhimisho ya miaka 30 mviwata

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 12 Disemba, 2023 amefungua Mkutano Mkuu wa 28 na Maadhimisho ya miaka 30 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) uliofanyika katika Ukumbi wa Agreement Mkoani Njombe.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia amewataka Wakulima nchini kuongeza kasi ya uzalishaji mazao kwakuwa Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inayo nia njema ya kuwaboreshea mazingira rafiki ikiwemo kuongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo kila mwaka.

Share: