Mahakama nchini Marekani imeamuru Mgahawa maarufu wa Swahili Village, kuwalipa Wafanyakazi wake fidia ya dola za Kimarekani Laki tano.
Mgahawa huo unaouza Chakula cha Kiswahili/Kiafrika na unaomilikiwa na raia wa Kenya Kevin Onyona, ulishtakiwa na Wafanyakazi 72 kwa kuwaibia na kuwadhulumu haki zao.
Dhulma hiyo iliyoendelea kwa miaka mingi ilihusisha mishahara ikiwemo malipo ya masaa ya ziada (overtime), haki ya kupumzika siku za kuugua n.k.
Mgahawa huo ulioanza rasmi mwaka 2016 una Matawi katika Majimbo kadhaa ikiwemo Maryland, Washington na New Jersey.
Watu wengi mashuhuri wamewahi kupata chakula katika mgahawa huo akiwemo Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyata na Rais William Ruto.
Pamoja na hukumu hiyo,Mgahawa huo umetakiwa kufuata sheria za ajira, kutoa ripoti za mara kwa mara na kuanzia sasa utafuatiliwa kwa karibu kwa miaka mitatu.