Marekani: mauzo ya silaha za kwenda nje ya nchi kwa mwaka 2023 yameongezeka kwa asilimia 56%

Wakati huo huo, Utawala wa Rais Joe Biden umesema kitendo cha kuiuzia silaha Ukraine, kinasaidia kukuza uchumi wa ndani wa Marekani.

Mauzo ya Silaha za kwenda nje ya nchi kwa Mwaka 2023 yameongezeka kwa 56% na kufikia Dola Bilioni 238 (Tsh. Trilioni 604) kulinganisha na mwaka 2022 huku vita ya Urusi dhidi ya #Ukraine ikizidisha mahitaji hayo

Poland ambayo ipo katika harakati za kupanua Jeshi lake, nayo ni kati ya Mataifa yaliyonunua Silaha nyingi zikiwemo Helikopta za Apache kwa Dola Bilioni 12 (Tsh. Trilioni 30), Mfumo wa  Roketi (Himars) Dola Bilioni 10 (Tsh. Trilioni 25), Dola Bilioni 3.75 (Tsh. Trilioni 9) kwa Vifaru vya M1A1 Abrams na Mfumo wa Ulinzi wa Anga Dola Bilioni 4 (Tsh. Trilioni 10)

Wakati huo huo, Utawala wa Rais Joe Biden umesema kitendo cha kuiuzia silaha Ukraine, kinasaidia kukuza uchumi wa ndani wa Marekani.

Share: