Kukamilika kwa Hospitali hii kutasaidia kupunguza gharama kwa Wakazi wa maeneo ya karibu kutembea umbali mrefu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea na mkakati wa kuboresha sekta ya afya nchini ili kusogeza huduma bora za afya karibu na Wananchi.
Akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa Hospitali ya Wilaya ya Rorya, mkoani Mara, Waziri Mkuu ameagiza kuendelea kukamilishwa kwa ujenzi wa Hospitali hiyo pamoja na kununua vifaa tiba ili kuimarisha hali ya utoaji huduma kwa Wananchi.
“Kukamilika kwa Hospitali hii kutasaidia kupunguza gharama kwa Wakazi wa maeneo ya karibu kutembea umbali mrefu hadi Tarime kufuata huduma za afya, Hospitali hii ni suluhisho”.
Ujenzi wa hospitali hiyo ambayo inajengwa kwa njia ya force account umeshatumia kiasi cha shilingi bilioni 3.25 kutoka Serikali kuu zilizotoka kwa awamu tatu na mwaka 2020 ilianza kutoa huduma mbalimbali za Wagonjwa wa nje ambapo inahudumia takribani watu 400 kwa mwezi.