Baadhi ya sababu zilizotajwa na EWURA kuchangia mabadiliko hayo ni kuongezeka kwa bei za Mafuta Yaliyosafishwa
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za mafuta zilizoanza kutumika leo Aprili 3, 2024 ambapo kuna ongezeko la bei kwenye Petroli na Dizeli huku Mafuta ya Taa bei ikibaki kama ilivyokuwa Machi 2024.
Upande wa Dar es Salaam bei ya Petroli ni Tsh 3,257 ikiwa ni ongezeko la Tsh 94, Dizeli ni Tsh. 3,210 kuna ongezeko la Tsh. 84, Mafuta ya Taa bei ni Tsh. 2,840 sawa na ilivyokuwa mwezi uliopita.
Baadhi ya sababu zilizotajwa na EWURA kuchangia mabadiliko hayo ni kuongezeka kwa bei za Mafuta Yaliyosafishwa (FOB) katika Soko la Dunia kwa wastani wa 3.94% kwa Petroli na wastani wa 2.34% kwa mafuta ya Dizeli, kuongezeka kwa kiwango cha kubadilishia Fedha za Kigeni kwa 3.19% kutokana na ongezeko la matumizi ya EURO kulipia mafuta yaliyoagizwa.