Mafuta yapanda bei mwezi machi

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano, tarehe 6 Machi 2024 saa 6:01 usiku. Kwa mwezi Machi 2024, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam petrol ni Tsh. 3163 kwa lita, dizeli Tsh. 3126 na mafuta ya taa 2840.

Mamlaka hiyo imesema Mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Machi 2024 yamechangiwa na ongezeko la bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia (FOB) kwa wastani wa asilimia 4.5 kwa mafuta ya petroli na asilimia 1.99 kwa mafuta ya dizeli na kupanda kwa gharama za uagizaji wa mafuta (premiums) kwa Bandari ya Dar es Salaam kwa wastani wa 15.38 kwa petroli na asilimia 40.41 kwa dizeli na kwa Bandari ya Mtwara kwa wastani wa asilimia 7.61 kwa petroli na dizeli. Mabadiliko ya bei za mafuta yamechangiwa pia na ongezeko la matumizi ya EURO katika kulipia mafuta yaliyoagizwa.

Share: