Lindi: ummy mwalimu awataka msd kupeleka dawa kilwa

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amepokea taarifa ya hali ya Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Lusajo Mwakajoka ambayo inaonyesha hali ya upatikanaji wa huduma za Afya katika Mkoa wa Lindi, upatikanaji wa Vifaa na Vifaa Tiba pamoja na changamoto.

Taarifa hiyo imeainisha changamoto mbalimbali ikiwemo suala la ajira za watumishi ambapo Mhe. Waziri Ummy amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuajiri watumishi wa mikataba kwa kutumia mapato ya ndani, hali ya upatikanaji wa dawa zipo kwa asilimia 87 na kuwataka MSD kuharakisha kupeleka dawa katika Wilaya hiyo.

Share: