Kurasa 365: waziri mifugo abdallah ulega ameupongeza mradi bbt kwa kuisaidia wizara hiyo kupiga hatua kwenye utendaji wa kazi

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameisaidia Wizara hiyo kwenye upande wa bajeti mara 4 zaidi ya bajeti waliyokua nayo kwa mwaka 2021/2022 huku akisema kwa upande wa mradi wa Building a Better Tomorrow (BBT) umezalisha faida ya zaidi ya Tsh. milioni 100.

Ulega ameyasema hayo mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye jukwaa la kilele cha wiki ya kurasa 365 za Mama Vol. 3 lililoandaliwa na CLOUDS MEDIA GROUP na kufanyika Mlimani City Dar es salaam kwa lengo la kumualika yale yote makubwa yaliyofanywa katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia.

Waziri Ulega amesema mradi wa BBT upande wa Mifugo na Uvuvi umefanya kazi nzuri kwenye vituo 8 na sasa vinaenda kuwa vituo 13 ambapo walinunuliwa ng’ombe 2,348 na waligawanywa kwenye vituo 8 ikiwemo Tanga, Mwanza na Kagera na tayari faida ya zaidi ya Tsh. milioni 100 imepatikana kwenye mradi huo.

Ulega amesema Mwaka 2021/2022 Wizara yao ilikua na bajeti ya bilioni 66.5 ambapo kwa sasa bajeti yao ni bilioni 295.9 ikiwa ni mara 4 zaidi, ambapo imeisaidia Wizara hiyo kupiga hatua kwenye utendaji wa kazi ambapo kwa sasa Tanzania imefanikiwa kupeleka nyama Nchi kama za Dubai na Saudia kitu ambacho miaka ya nyuma hakikuwahi kuwepo.

Mbali na hiyo Waziri Ulega amesema minada 51 imejengwa yenye thamani ya bilioni 17.5 na ng’ombe zaidi milioni 12 wameuzwa kwenye minada hiyo na tayari Wizara imepata ithibati ya mbegu za malisho ambazo Wafugaji wataenda kununua kwa ajili ya kipindi cha kiangazi ili Wafugaji wasikose malisho “Tanzania siku zijazo itaacha kuagiza Vifaranga vya nyama wala mayai sababu tayari shamba la Kuku Wazazi lililopo Siha linakwenda kuzalisha mayai vifaranga 1,200 na hii ni kutokana na kuku kupendwa sana”

Share: