Kongamano la uwekezaji kufanyika machi 27

Kongamano hilo ni mwendelezo wa uhusiano mzuri wa kidiplomasia baina ya nchi hizo ambapo mwaka huu zinatimiza miaka 60 ya ushirikiano.

KATIKA kile kinachothibitisha kuwa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan umefungua fursa za kiuchumi Machi 27, 2024 kampuni 180 za China na Tanzania zinatarajiwa kufanya kongamano la uwekezaji na biashara hapa nchini.

Kongamano hilo ni mwendelezo wa uhusiano mzuri wa kidiplomasia baina ya nchi hizo ambapo mwaka huu zinatimiza miaka 60 ya ushirikiano.

Mwamanga ametoa wito kwa kampuni za Tanzania kujitokeza kwa wingi katika kongamano hilo ambalo litakuwa na fursa nyingi za uwekezaji.

Ofisa huyo amesema kampuni hizo 60 zimelenga kuja kuangalia maeneo ya uwekezaji kwenye sekta ya afya, kilimo,, vifaa vya ujenzi madini, mazao ya kilimo na viwanda.

Mwamanga amesema kwa sasa China inashika nafasi ya kwanza kwa uwekezaji Tanzania na mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano mzuri uliopo kati Tanzania.

Kwa upande wake Meneja Maendeleo ya Wanachama Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Kelvin Ogodo amesema sekta binafsi imejipanga kikamilifu ili kuweza kunufaika na ujio huo wa wageni kutoka China.

Share: