Vifaranga waliochomwa moto katika zoezi lililosimamiwa na iliyokuwa Mamlaka ya Dawa na Chakula nchini Tanzania (TFDA) Mwaka 2017
Katika Kikao cha siku mbili kilichofanyika kuanzia Aprili 29 hadi 30 katika makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha, Tanzania, wataalamu wa sekta ya ufugaji na ututoaji wa vifaranga wamesema kuwa kikundi chochote kitakachonuia kusafirisha bidhaa za kuku kati ya nchi hizo mbili kufanya tathmini ya hatari na kuhakikisha kuwa hatua za usafi zinazingatiwa.
Mwaka 2017, mamlaka za Tanzania zilichoma moto mzigo uliosheheni vifaranga 6,400 kutoka nchini Kenya, hatua iliyotia dosari uhusiano wa kibiashara baina ya majirani hao.
Vifaranga hao walichomwa moto upande wa Tanzania katika zoezi lililosimamiwa na iliyokuwa Mamlaka ya Dawa na Chakula nchini Tanzania (TFDA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).