Kenya inampango wa kutengeneza kinu cha kwanza cha nishati ya nyuklia nchini humo

Kenya itahitaji walau bilioni 11 (dola milioni 83) kama gharama ya awali ya kutengeneza kinu cha kwanza cha utafiti wa nishati ya nyuklia nchini humo.

Haya yanajiri baada ya timu ya wataalamu kutoka Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kusema kuwa nchi hiyo imepiga hatua kubwa katika maendeleo ya miundombinu ya nyuklia.

Kenya inatarajia kuzindua mradi huo kati ya 2030 na 2034 huku ujenzi wake ukianza mwaka 2026.

Hadi kukamilika kwake, mradi huo utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 1,000.

Share: