Kassim Majaliwa: Mradi wa julius nyerere wafikia asilimia 96.8% na utazalisha megawati 2,115 za umeme

Amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akisoma hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025.

"Mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere ambao utazalisha Megawati 2,115 utekelezaji wake umefikia asilimia 96.81. Kama mlivyoshuhudia zoezi la kuwasha mtambo wa kuzalisha umeme lilifanyika kwa mafanikio na kufanikiwa kuingiza kwenye Gridi ya Taifa Megawati 235. Mtambo huo ni mmoja kati ya mitambo tisa itakayozalisha umeme katika mradi huo. Aidha, kazi zote katika mradi huu zinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Desemba, 2024."

Amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akisoma hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025.

Share: