Kampuni ya twiga mchango wake katika sekta ya madini

Kampuni ya Madini ya Twiga imetumia dola bilioni 3.041 (Sh7.5 trilioni) ikiwa ni mchango wake katika uchumi wa Tanzania tangu lilipoanzishwa miaka mitatu iliyopita.

Takwimu hizo zimetolewa juzi wakati wa Kongamano la Madini na Uwekezaji Tanzania 2023.

"Hii imetutambulisha kama mlipaji mkubwa wa gawio kwa Serikali na mchangiaji mkubwa wa uchumi kupitia kodi, ajira na miradi ya jamii," amesema Dk. Mark Bristow, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barrick.

Kwa mujibu wa takwimu hizo zilizoanzishwa Septemba 2019 hadi Septemba mwaka huu, malipo ya gawio na mkopo yalikuwa dola 158milioni,

mishahara dola 227milioni, watoa huduma wazawa dola 150Omilioni, na miradi ya kijamii dola 13.2milioni, Pia kodi mrabaha, tozo na malipo yalikuwa dola 1,097bilion.

Hatua hiyo inajitokeza baada ya Barrick na Serikali kuunda kampuni ya Twiga Oktoba 2019 inayosimamia migodi mitatu iliyokuwa chini ya kampuni ya Acacia.

Kwenye kampuni hiyo mpya Barrick inamiliki asilimia 84 ya hisa zote huku Serikali ikiwa na asilimia 16. Utaratibu huo ni utekelezaji wa sheria mpya ya madini iliyopitishwa mwaka 2017.

Hata hivyo, mshauri wa nishati mpito Afrika kutoka Shirika la Kufuatilia Usimamizi wa Rasilimali za Asili (NRGI), Silas Olang amesema si rahisi kujua Tanzania imenufaika kwa kiwango ilichostahili kupitia takwimu hizo.

"Wanatakiwa watujulishe ni kiasi gani cha madini walichozalisha na kuuza pia si sahihi kuhesabu ajira katika uchangiaji kwa sababu ilikuwa ni sehemu ya uokoaji wa gharama,"

alisema kuhusu mageuzi hayo yaliyotokana na uongozi wa Rais John Magufuli, mwaka 2017 enzi za uhai wake.

Share: