Joseph kusaga amefanya mazungumzo na balozi wa china nchini tanzania

Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds media group Joseph Kusaga amekutana nakufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian.


Kusaga ameshukuru mazungumzo hayo ya kina na Balozi wa China ambapo lengo lake kuu likiwa ni kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na China.

"Tumejitolea kama kawaida, Longping na Clouds Media Group wanaendelea kutafuta maendeleo ya kilimo kwa ajili ya jamii zetu, shukrani za dhati kwa Ubalozi wa China kwa ukarimu wao" Joseph Kusaga

Share: