Jamila Mbarouk: niwahakikishie watanzania kwamba tutatumia muda uleule tuliowaahidi wa dk 90 dar - morogoro

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limewahakikishia Watanzania kwamba safari za treni ya umeme zitakapoanza rasmi mwezi July mwaka huu abiria watatumia saa tatu tu kutoka Dar es salaam hadi Dodoma ambapo jana wakati wa safari ya kwanza ya majaribio treni hiyo imetumia saa nne kutoka Dar hadi Ddooma ambapo iliondoka saa 10 kasoro jioni na kufika Dodoma saa 1 usiku.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano - TRC, Jamila Mbarouk amesema “Dar es salaam hadi Dodoma kwa safari hii ya kwanza ya majaribio tumetumia masaa manne lakini baada majaribio kukamilika tutatembea masaa matatu kwa kuwa tutakuwa na vituo lakini kama tukitembea one way bila kusimama kwenye vituo tunafika chini ya masaa matatu”

Itakumbukwa safari ya mwisho ya majaribio kutoka Dar es salaam hadi Morogoro treni hiyo ilitumia muda chini ya masaa mawili ambapo Jamila alisema “Safari hii tumetumia muda chini ya masaa mawili, kila siku tunavyoendelea kufanya majaribio ya miundombinu kwa lengo la kuangalia mifumo ya umeme na ufanisi wa uendeshaji umeme, niwahakikishie Watanzania kwamba tutatumia muda uleule tuliowaahidi wa dk 90 Dar - Morogoro na masaa matatu Dar - Dodoma”



Share: