Iringa: kasesela amesisitiza kuhusu nidhamu ya fedha ili kufikia mafanikio ya kila mmoja anayetamani kufanikiwa

Mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM ndugu Richard Kasesela amesisitiza kuhusu nidhamu binafsi na nidhamu ya fedha ili kufikia mafanikio ya kila mmoja anayetamani kufanikiwa.

Kasesela ametoa kauli hiyo leo alipokuwa mgeni wa heshima kwenye kufunga mafunzo ya awamu ya kwanza ya ujasiriamali wa kilimo cha matunda,mafunzo yaliyoandaliwa na chuo kikuu cha Iringa.

Mafunzo hayo yamejumuisha wanafunzi zaidi ya 200 kutoka kwenye mikoa minne ya Morogoro, Iringa, Njombe na Mbeya yakidhaminiwa na taasisi ya Feed the future kwa hisani ya watu wa Marekani.


"Tumeletwa duniani kwa mambo mawili,kuabudu Mungu na kutafuta fedha",amasema mjumbe huyo wa NEC na mkuu wa wilaya wa zamani wilayani Iringa.

Aidha Kasesela aliongeza kusema "nidhamu ndiyo msingi wa mafanikio ya wengi, Nidhamu binafsi, nidhamu ya fedha,nidhamu katika kuheshimu taifa lako na nidhamu ya jumla kwa jamii na nidhamu ya kutunza muda"

Katika hafla hiyo pia mkulima wa Ilula Athuman Mohamed wa Ruaha Mbuyuni mwenye ulemavu wa mguu alipata udhamini wa magongo ya kutembelea huku Kasesela akiwaomba wadau wamsaidie apate walau power tiller ya kumsaidia kwenye shughuli zake za kilimo.

Share: