Imegundulika uwepo wa madini ya nikeli (nickel) liparamba nchini tanzania

Kampuni ya Resource Mining Corporation Ltd (ASX:RMI) imegundua uwepo wa madini ya nikeli (nickel) na shaba (copper sulphide) katika Mradi wa Nickel wa Liparamba nchini Tanzania, hii ikiwa ni uthibitisho wa kwanza wa uwepo wa madini hayo katika eneo hilo.

Kampuni hiyo ambayo imejikita katika uchimbaji wa madini ya kutengenezea betri ilifanya ugunduzi huo mwezi Septemba 2023.

Kampuni hiyo ya Australia pia itafanya mapitio ya matokeo hayo ili kuamua ni programu zipi za uchunguzi zaidi zitakazofanywa ndani ya maeneo ya miradi ya sasa na kwa eneo kubwa zaidi.

Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Asimwe Kabunga ameeleza kuwa kugunduliwa kwa madini hayo ndani ya Mradi wa Nickel wa Liparamba ni matokeo mazuri na yanaleta fursa ya kusisimua kwa kampuni yao.

Share: