Ethiopia: wateja wa benki ya cbe walitoa fedha kwa kiwango kikubwa kuliko kiwango kilicho ndani ya akaunti zao

Shida ya mfumo iliyotokea katika Benki ya Biashara (CBE) imesababisha Wateja wa Taasisi hiyo kutoa fedha kwa kiwango kikubwa kuliko kiwango kilicho ndani ya akaunti zao

Inadaiwa shida hiyo ya Mtandao ilianza kugunduliwa na Wanafunzi wa Vyuo kuanzia Saa 7 Usiku na zoezi hilo likaendelea hadi Saa 8 Usiku ikidaiwa zaidi ya Dola Milioni 40 (Tsh. Bilioni 102) zilitolewa au kuhamishiwa kwenda wa benki nyingine

Imeelezwa kuwa kulikuwa na foleni ndefu kwenye ATM za Vyuo hadi Maafisa wa Polisi walipofika kuwazuia. Zaidi ya Watu Milioni 38 wana Akaunti katika Benki hiyo ya CBE ambayo ilianzishwa Miaka 82 iliyopita

Share: