Dkt. natu mwamba ateta na mkurugenzi mkazi wa benki ya dunia

Ikumbukwe kwamba Tanzania ni mwana hisa wa taasisi hiyo kubwa ya fedha duniani

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete, ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo wamejadiliana mambo kadhaa yanayohusu ushirikiano kati ya Tanzania na Benki hiyo. 



Ikumbukwe kwamba Tanzania ni mwana hisa wa taasisi hiyo kubwa ya fedha duniani, ambapo Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ni miongoni mwa magavana wa Benki hiyo, huku Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, ni magavana mbadala (Alternate Governors) wa benki hiyo.

Share: