Dkt. festo dugange amekanusha taarifa ya kituo cha afya kugharimu bil 2.3

kutokana na maelezo ya kina kuhusu andiko iliyowasilishwa Bungeni Aprili 15, 2024 akidai kiasi hicho ni kikubwa

Mbunge wa Viti maalumu, Hawa Mwaifunga amehoji matumizi makubwa ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mahoma Nyika mkoani Dodoma ambapo amesema ujenzi wa kituo hicho unagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 2.3 kutokana na maelezo ya kina kuhusu andiko iliyowasilishwa Bungeni Aprili 15, 2024 akidai kiasi hicho ni kikubwa.

Mwaifunga amesema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 Bungeni jijini Dodoma.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi (Afya), Dkt. Festo Dugange amekanusha taarifa hiyo akisema ilipelekwa kwenye kamati kama wasilisho la 'draft' ya bajeti na hatua imeshachukuliwa kuwa fedha hizo bado hazijatumika na pindi zikitumika zitazingatia thamani ya mradi. 

Share: