Amewapongeza Wakandarasi wa umeme Vijijjni waliofanya kazi ya usambazaji Mkoani Iringa
Serikali imesema usambazaji umeme Vijijini Mkoani Iringa umefanyika kwa asilimia 100 ambapo Vijiji vyote 360 Mkoani humo vimesambaziwa umeme kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema hayo akiwa Mkoani Iringa kwa ajili kuwasha umeme na kukagua miundombinu ya umeme ambapo amesema usambazaji umeme katika Vitongoji vya Mkoa huo umetekelezwa kwa asilimia 64.11 na Vitongji 1,188 vimesambaziwa umeme kati ya 1,853.
Baada ya kuwasha umeme kwenye Kijiji cha Mkangwe Wilayani Mufindi, Dkt. Biteko amewataka Wakandarasi wa miradi ya usambazaji umeme Vijijini kutekeleza kazi kwa wakati ili kuendana na kasi ya maendeleo huku akiiagiza REA kuwachukulia hatua Wakandarasi wazembe.
Amewapongeza Wakandarasi wa umeme Vijijjni waliofanya kazi ya usambazaji Mkoani Iringa ambayo imepelekea Vijiji vyote Mkoani humo kuwa na umeme hadi kufikia December 2023.