Ded iringa apewa wiki mbili kuwasilisha mpango wa kukamilisha shule ya sekondari mlenge

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde amempa wiki mbili Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini, Bashir Muhoja kuwasilisha mpango mkakati wa kukamilisha ujenzi wa Shule ya Sekondari Mlenge. 

Dkt. Msonde ametoa maelekezo hayo mapema leo mara baada ya kukagua maendeleo ya shule hiyo inayojengwa kupitia mradi wa SEQUIP ambapo Sh.Milioni 470 zimetolewa.

"Kuna baadhi ya maeneo ambayo shule zilizojengwa kupitia mradi wa SEQUIP hazijakamilika lakini si kwa kiwango cha chini kama cha Shule ya Sekondari Mlenge, kwani katika maeneo mengine ujenzi wa shule umekamilika kila jengo isipokuwa miundombinu ya ndani ya maabara, au rangi haijapigwa."

“DED hakikisha majengo haya yanakamilika mapema iwezekanavyo na ndani ya wiki mbili uwasilishe kwa Katibu Mkuu OR- TAMISEMI mpango mkakati wa namna ya ujenzi wa shule hii utakavyokamishwa,” amesema Dkt. Msonde. 

Amesisitiza kuwa shule zote zinapaswa kukamilika ndani ya mwaka huu wa fedha ili kuunga mkono dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuboresha miundombinu ya elimu nchini.

Share: