Dar es salaam yaongoza kwa idadi kubwa ya usajili wa huduma za mawasiliano

Mtandao wa Vodacom umefikisha Wateja 21,272,484 (30%) ukifuatiwa na tiGO wenye Wateja 19,698,263 (28%), Airtel 19,146,016 27%, Halotel 8,529,919 (12%) na TTCL 1,644,194 (3%).

Ripoti ya Robo ya Mwisho wa Mwaka 2023 inayoangazia Huduma za Mawasiliano Nchini, imeonesha hadi kufikia Desemba 2023, jumla ya Wateja 70,290,876 wa Huduma za Mawasiliano walisajiliwa, ikiwa ni ongezeko la 4.7% kutoka Wateja Milioni 67.1 waliokuwepo Septemba 2023.

Mkoa wa Dar es Salaam umeongoza kwa idadi kubwa ya Usajili wa Huduma za Mawasiliano ikiwa na Wateja Milioni 12.9 (18.4%). Mwanza unafuatia ukiwa na 6.6%, Arusha 6.0%, Mbeya 5.8%, Dodoma 5.3%. Mikoa ya yenye Wateja chini ya 100,000 kila mmoja ni Kusini Unguja na Kaskazini Unguja.

Mtandao wa Vodacom umefikisha Wateja 21,272,484 (30%) ukifuatiwa na tiGO wenye Wateja 19,698,263 (28%), Airtel 19,146,016 27%, Halotel 8,529,919 (12%) na TTCL 1,644,194 (3%).

Share: