Makubaliano hayo ni ya kwanza ya aina yake na yanaashiria mwanzo wa mwisho wa enzi ya matumizi ya mafuta.
Wawakilishi kutoka takriban nchi 200 wanaoshiriki mkutano wa kilele wa kimataifa wa Mazingira COP28 mjini Dubai, wamekubaliana leo kuanza kupunguza matumizi ya nishati za visukuku, ili kuepusha madhara ya tabia nchi.
Makubaliano hayo ni ya kwanza ya aina yake na yanaashiria mwanzo wa mwisho wa enzi ya matumizi ya mafuta.
Makubaliano hayo yametangazwa na Mkuu wa shirika la kitaifa la mafuta katika Umoja wa Falme za Kiarabu Sultan Al Jaber ambaye ndiye rais wa mkutano huo mwaka huu.
Makubaliano hayo yanakusudia kutuma ishara yenye nguvu kwa wawekezaji na watunga sera kwamba dunia sasa imeungana kuachana na mafuta, jambo ambalo wanasayansi wanasema ni tumaini bora la mwisho kuzuia janga la hali ya hewa.