Chmt yatakiwa kusimamia ufungaji vifaa tiba hospitali ya morogoro dc

Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais -TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume ameitaka Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya(CHMT) kuhakikisha vifaa na vifaa tiba vyote vilivyopelekwa Hospitali ya Wilaya ya Morogoro Vijijini kufungwa kutumika kwa kutoa huduma kwa wananchi.

Dkt. Mfaume akizungumza na timu hiyo na watumishi wa afya alipokuwa akikagua ujenzi na huduma zinazotolewa hospitalini hapo.

Mkurugenzi huyo amesema hospitali imeanza kufanya kazi lakini baadhi ya vifaa na vifaa tiba vilivyopelekwa havijafungwa ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Aidha, amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu akieleza takwimu kuonesha wilaya hiyo ina changamoto ya viashiria vya upotevu mkubwa wa bidhaa za afya.

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Robert Manyerere amesema hospitali hiyo ni msaada kwa wakazi 387,736 wa Halmashauri hiyo.

Share: