Changamoto ya umeme suluhu kupatikana april mwaka huu

Rais Samia Suluhu Hassan amesema tatizo la upungufu wa umeme litakwenda kupata suluhu yake mwezi April mwaka huu wa 2024 baada ya megawati 470 hadi 500 zitazozalishwa katika Bwawa la Mwalimu Nyerere kuingizwa kwenye gridi ya Taifa.

Akiongea na Watanzania waishio Ughaibuni akiwa Nchini Italy kwenye ziara aliyoifanya hivi karibuni, Rais Samia amenukuliwa akisema “kuhusu sababu za upungufu wa umeme ni kwasababu kwa muda mrefu mitambo yetu ya umeme haikuwa imefanyiwa ukarabati na pili uwekezaji na matumizi ya umeme majumbani umezidi mno, tumefanya mradi wa kusambaza umeme Vijijini huko na Vitongoji, sasa matumizi ya umeme yamezidi kukua lakini vyanzo ni vilevile hatujaongeza, tumeongeza vyanzo kidogo pale kinyerezi kwa umeme wa gesi lakini uwekezaji nao ni mkubwa mno”

“Sasa tatizo hili linakwenda kupata suluhu yake, sio Suluhu Mimi ni suluhu ya umeme nadhani April mwaka huu kwasababu kwenye lile Bwawa ambalo tungetarajia lingezalisha megawati 2115 tunakwenda kuzalisha megawati kama 500 au 470 April, lile Bwawa litaendeshwa na mota 9, tunakwenda kuwasha mbili, April mbili zitawaka na kila moja inakwenda kutoka megawati kama 250 na zaidi kwahiyo tunategemea megawati 470 mpaka 500 zitakwenda kuingia kwenye gridi ya Taifa na kupunguza changamoto ya umeme, kwahiyo kwenye umeme suluhisho linakwenda kupatikana”

Share: