Chalamila: serikali imetenga bilioni 16 mradi wa kupitisha umeme chini ya ardhi

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametaja miongoni mwa sababu za kukatika umeme katika baadhi ya maeneo, huku akisema Rais wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha kwa ajili ya upitishwaji wa umeme wa ardhini (underground cable) ambapo awamu ya kwanza unatoka Ilala kwenda kurasini wenye urefu wa kilomita 6.8 uliogharimu shilingi bilioni 16.

“Ukweli usiopingika kwamba nchi yetu kwa muda mrefu uwekezaji umekuwa, makazi yamekuwa lakini vyanzo vya umeme ni vilevile ya tangu zamani, kinachotokea ni kitu gani hii njia ni kama wale watu anachukua gari anatoa redio ya zamani anaweka lile lispika kubwa halafu kawaya anakokatumia kanakuwa kadogo ambapo baada ya muda unakuta kale kawaya kanaungua moto, kilichopo hapa ni kwamba umeme wanao lakini unafikaje kwa wananchi waliozagaa wengi ukiusafirisha umeme wote paap!!!

Kwa miundombinu ile ile iliyopo nyaya zinaanza kuelemewa, mitambo inaanza kuelemewa jamaa kule wanaambiwa jamani eeh punguzeni umeme vinginevyo utaunguza zile njia za kusafirishia, sasa nini kifanyike serikali imesema tupitishe njia nyingine tena ya umeme lakini kwa kuwa Mji wetu wa Dar es Salaam ni jiji tunataka uwe mji mzuri tuachane na uchafu huu wa manguzo nguzo twende sasa chini, tupitishe chini ambapo hakutakuwa na matatizo ya aina yoyote sasa mradi huu wa kupitisha chini utatumia Bilioni 16 ambapo ni fedha nyingi sana na njia hii hadi mwezi wa tatu itakuwa imekamilika,”

Share: