Chalamila: dar es salaam kuanza mchakato wa leseni za kufanya biashara masaa 24

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema wanakamilisha mchakato wa kuanza biashara saa 24 katika Jiji la Dar es salaam ambapo wataandaa mfumo mpya ambao utahusisha leseni ambazo zitasaidia Watu kufanya biashara saa 24.

Akiongea leo Jijini Dar es salaam, Chalamila amesema “Dar es salaam ni Mji Mkubwa wakati huu tunapojiandaa kuanza biashara masaa 24 kwa kukamilisha Soko la Kariakoo, Timu zetu zipo kwenye mazungumzo sasa kwenye vikao vya awali, Taasisi za fedha, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wasafirishaji, Wafanyabiashara. TANESCO, DAWASA pamoja na Mamlaka nyingine zote tunakamilisha mchakato wa kufanya biashara saa 24”

“Tumeweka mfumo mpya tutakapotoa leseni, leseni hizo zitatusaidia kufanya biashara saa 24, hali ya ulinzi na usalama imeendelea kuboreshwa”



Share: