Cag: ucheleweshwaji wa miradi ya barabara umechangia kuongezeka kwa gharama

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema changamoto za kuchelewa kukamilika kwa Miradi ya Barabara kumechangia kuongezeka kwa gharama za Miradi

Amesema “Tulichukua Miradi Mitano ya Barabara za TANROADS na kubaini gharama iliongezeka kwa zaidi ya Tsh.Bilioni 185. Ongezeko hili lilisababishwa na sababu mbalimbali, kubwa Mbili ni upembuzi na usainifu wa kina usio sahihi. Hii ilisababisha ongezeko la Tsh. Bilioni 44.97 sawa na 34% ya gharama zote za ziada"

Ameongeza “Pili ni kucheleweshwa kwa Miradi na malipo ya Wakandarasi na Washauri elekezi. Hii imesababisha ongezeko la gharama la Tsh. Bilioni 85.53 sawa na 66%. Kuchelewa kwa mradi inasababisha Wahusika wanaanza kudai na wakati huohuo wanaendelea kulipwa."

Share: