Cag: ripoti ya mwaka wa fedha wa 2022/23 imebaini taasisi nne za serikali zilitumia tsh. bilioni 10.20 zaidi ya bajeti iliyopitishwa

CAG anaeleza matumizi ya fedha katika kutekeleza shughuli ambazo hazijapangwa kunaathiri utekelezwaji wa shughuli zilizopangwa

Kifungu cha 27 (4) cha Sheria ya Bajeti Sura ya 439 Toleo la Mwaka 2020 kinataka matumizi yaliyoidhinishwa kwa Serikali na Taasisi za Umma yafanyike kulingana na madhumuni yaliyoelekezwa na kwa mujibu wa mipaka iliyowekwa na makadirio yaliyopo

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG kwa Mwaka wa Fedha wa 2022/23 imebaini Taasisi Nne za Serikali zilitumia Tsh. Bilioni 10.20 kama malipo ya matumizi ya kawaida na maendeleo zaidi ya Bajeti iliyopitishwa

CAG anaeleza matumizi ya fedha katika kutekeleza shughuli ambazo hazijapangwa kunaathiri utekelezwaji wa shughuli zilizopangwa, pia kunaweza kuchangia uwepo wa matumizi yasiyo na tija kwa Serikali

Anapendekeza Serikali na Mamlaka zinazohusika kuzingatia Sheria ya Bajeti na Kanuni zake ili kuwezesha upatikanaji wa thamani ya fedha

Share: