Bodi ya stamigold kuongeza ufanisi wa mgodi

Serikali imeitaka Bodi ya Wakurugenzi ya STAMIGOLD kuweka mikakati itakayosaidia kuongeza ufanisi wa mgodi na kusimamia malengo ya mgodi huo ikiwa ni pamoja kuongeza uzalishaji kufikia wakia 1,500 na kufanya utafiti kuongeza uhai wa mgodi.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo,wakati akizungumza katika kikao na Bodi ya Wakurugenzi ya STAMIGOLD, ambayo ni Kampuni tanzu ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Amesema kuwa Bodi hiyo ina wajibu muhimu wa kuhakikisha kuwa malengo hayo muhimu yanatekelezwa kikamilifu na kwamba kwa kufanya hivyo, watasaidia kuhakikisha ukuaji endelevu wa shughuli za mgodi na kampuni kwa ujumla.

Mbibo amesema kuwa miongoni wajumbe wanaounda Bodi hiyo kuna wataalam mbalimbali wenye mchango mkubwa kwenye Sekta ya Madini hivyo ni matumaini kuwa watatoa ushirikiano mkubwa kwa menejimenti ya STAMIGOLD kwa namna ya kutekeleza majukumu yao.

Share: