Aidha mkoani Tanga bei ya petroli ni shilingi 3,064 na dizeli ni shilingi 3,219 huku mkoani Mtwara petroli itauzwa shilingi 3,201 na dizeli itauzwa shilingi 3,456.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Nchini (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta ambazo zimeshuka ikilinganishwa na mwezi uliopita.
Bei ya mafuta ya petroli imeshuka kutoka shilingi 3,158 Desemba 2023 hadi shilingi 3,084 Januari 2024 katika Mkoa wa Dar es Salaam, huku ya dizeli ikishuka kutoka Sh3,226 hadi Sh3,078 katika kipindi kama hicho.
Aidha mkoani Tanga bei ya petroli ni shilingi 3,064 na dizeli ni shilingi 3,219 huku mkoani Mtwara petroli itauzwa shilingi 3,201 na dizeli itauzwa shilingi 3,456.
"Kupungua kwa bei za mafuta kwa Januari 2024 ni kwa sababu ya kushuka kwa bei za mafuta (FOB) katika soko la dunia kwa wastani wa asilimia 6.03 kwa petroli na asilimia 7.13 kwa dizeli, pia kupungua kwa bei za mafuta kumetokana na kushuka kwa gharama za uagizaji wa mafuta kwa wastani wa asilimia 3.72 kwa petroli, na asilimia 17.52 kwa dizeli kwa bandari ya Dar es Salaam".