Bashungwa akutana na bodi ya mfuko wa barabara kujipanga kimkakati

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) amekutana na Menejimenti ya Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) kujadili na kuweka mipango ya kuboresha utendaji kazi na Utekelezaji wa Majukumu ya bodi hiyo.

Kikao hicho kimefanyika Jijini Dodoma na kuhudhuliwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Eng. Godfrey Kasekenya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour, Naibu Katibu Mkuu Bw. Ludovick Nduhiye pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya Ujenzi.

Share: