Baraza la uuguzi na ukunga lafuta matokeo ya mtihani wa usajili na leseni kwa watahiniwa 1,330 wa stashahada

Watahiniwa hao watapewa nafasi ya kufanya Mtihani mwingine Februari 16, 2024 bila malipo yoyote na hawatahitajika kujisajili tena ambapo Mtihani utafanyika Dodoma.

Taarifa ya Wizara ya Afya imeeleza kuwa Mnamo Septemba 7, 2023, Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania liliendesha Mitihani ya Usajili na Leseni ambao Wizara hiyo ilibaini Mtihani ulivuja na kusambaa kwa Watahiniwa wa Stashahada hali iliyosababisha Watahiniwa 1,330 kufutiwa matokeo

Watahiniwa hao watapewa nafasi ya kufanya Mtihani mwingine Februari 16, 2024 bila malipo yoyote na hawatahitajika kujisajili tena ambapo Mtihani utafanyika Dodoma.

Aidha, Mtuhumiwa aliyehusika katika uvujishaji wa Mtihani huu tayari amesimamishwa kazi huku taratibu za Kinidhamu na Kisheria zikiendelea

Share: