Barabara ya tanga kilosa mikumi kupandishwa kuwa barabara kuu

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi kuipandisha hadhi barabara ya Tanga - Kilosa - Mikumi - Lupembe kuwa barabara kuu ‘Trunk Road’ ili kuinua uchumi wa mikoa ya Tanga, Morogoro na Njombe.

Bashungwa, ameyasema hayo mkoani Morogoro wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Dumila-Kilosa-Ulaya-Mikumi (km 142) kwa kiwango cha lami sehemu ya pili, Rudewa-Kilosa (km 24), ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 98.

“Barabara inayoanzia Tanga bandarini kupitita Handeni - Mziha - Dumira - Kilosa - Mikumi - Ifakara mpaka Lupembe mkoani Njombe lazima tuitangaze iwe ni mojawapo ya barabara kuu ‘Trunk road’ ili iweze kuipatiwa bajeti ya kutosha na kuweza kuihudumia wakati wote”, amesema Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amemtaka Mkandarasi M/s Umoja - Kilosa Jv anayetekeleza mradi huo kufanya kazi usiku na mchana na kuhakikisha barabara na madaraja yanakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa kwenye mkataba kwani fedha zote zimeshalipwa na ifakapo mwezi wa nne mwishoni waikabidhi barabara hiyo kwa wananchi.

Share: