Bajeti ya 2024/25  ni trilioni 47

washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia TZS trilioni 4.29 na mikopo ni TZS trilioni 8.3.

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema serikali inatarajia kukusanya na kutumia TZS trilioni 47.4 katika bajeti ijayo. Mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa TZS trilioni 34.4, washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia TZS trilioni 4.29 na mikopo ni TZS trilioni 8.3.

Mwigulu amesema hayo bungeni akiwasilisha mapendekezo ya mwongozo wa maandalizi ya mpango wa bajeti ya mwaka 2024/25.

Share: