Ajira zenu zipo palepale

Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, amewahakikishia usalama wa ajira zao watumimishi zaidi ya 276 waliokua wanafanyakazi chini ya kampuni ya KADCO iliyokua ikiendesha shughuli zake katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa zaidi ya miaka 25.

Kauli hiyo ya Prof. Mbarawa imekuja baada ya uwanja huo wa KIA kurudishwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege nchini (TAA)ambapo serikali kupitia Bunge iliitaka serikali isimamie kiwanja hicho cha ndege ili kuongeza ufanisi na tija katika sekta ya uchukuzi na utalii.

Akizungumza na watumishi hao Prof.Mbarawa amesema mabadiliko yaliyofanyika hayata athiri ajira ya mtumishi yeyote kwani serikali inatambua jitihada zao katika kukuza maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Amesema serikali imefanya hivyo kwa nia njema lengo likiwa ni kuboresha utoaji wa huduma bora zaidi hususani ya miundombinu ya uwanja huo ikiwemo taa, uzio pamoja na kujenga jengo la kusubiria (terminal three) la kisasa ili kukuza utalii wa ndani na nje ya nchi.

Share: