Mkoani Tanga imefanya Ukaguzi wa leseni za biashara katika kipindi cha Julai- Septemba, 2024 na kubaini Asilimia 64.35 hawakuwa na leseni za Biashara huku zaidi ya 90% ya wafanyabiashara hawakuwa wamelipa ushuru wa huduma (Service Levy) pamoja na Ushuru wa nyumba za kulala wageni (Hotel Levy)
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani humo Ramadhani Ndwatah wakati akizungumza na Vyombo vya habari Jijini Tanga ambapo amesema hatua zilizochukuliwa ni kufanya uelimishaji kwa wadau juu ya matakwa ya sheria juu ya ulipaji wa tozo hizo pamoja na madhara yake kwao.
Amesema matokeo ya mwitikio wa Wadau katika Utekelezaji wa hatua hizo kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2024, Halmashauri ya Jiji la Tanga iliweza kukusanya kiasi cha Shilingi 1,938,185,915.22 katika vyanzo vya ushuru wa huduma (Service Levy), nyumba ya kulala wageni (Hotel levy) pamoja na ada za leseni za Biashara (Business License Fee) ikilinganishwa na kiasi cha Shilingi 1,246,611,579.43 kilichokusanywa katika kipindi April hadi Juni 2024 katika vyanzo hivyo.
Share: