Mwaka 2023, Fico aliendesha kampeni iliyokosoa uungwaji mkono wa Nchi za Magharibi kwa Ukraine na kuahidi kukomesha msaada wa Kijeshi wa Slovakia kwa Ukraine
Waziri Mkuu wa Slovakia, Robert Fico yupo katika hali tete kiafya baada ya kujeruhiwa katika jaribio linalodaiwa kulenga kukatisha uhai wake
Inaelezwa ameshambuliwa kwa risasi nne alipokuwa nje ya Nyumba ya Utamaduni katika Mji wa Handlova, Machi 15, 2024, ambapo Polisi wamefanikiwa kumdhibiti mshambuliaji aliyekuwa katika kundi la Watu waliosubiri kumsalimia kiongozi huyo
Mwaka 2023, Fico aliendesha kampeni iliyokosoa uungwaji mkono wa Nchi za Magharibi kwa Ukraine na kuahidi kukomesha msaada wa Kijeshi wa Slovakia kwa Ukraine. Pia, hakuficha hisia zake dhidi ya Kremlin (Urusi) na kulaumu Ukraine kwa kumchokoza Rais Vladimir Putin