TRUMP: UKRAINE INAWEZA KUYAKOMBOA MAENEO YAKE YOTE YALIYOTEKWA NA URUSI

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema Ukraine ina uwezo wa “kurejesha ardhi yake yote na kuirudisha katika hali ya awali,” kauli inayotafsiriwa kama mabadiliko makubwa katika mtazamo wake kuhusu vita na Urusi.

Kupitia ujumbe aliouweka kwenye jukwaa lake la kijamii, Truth Social, Trump alibainisha kuwa Kyiv inaweza kufikia “mipaka yake ya asili, pale ambapo vita vilianzia,” endapo itapata msaada thabiti kutoka Ulaya na jumuiya ya NATO, hasa wakati ambapo uchumi wa Urusi unakabiliwa na shinikizo kubwa.


Kauli hiyo ilitolewa mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, yaliyofanyika baada ya Trump kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York siku ya Jumanne.

Ingawa amesisitiza mara kwa mara kwamba lengo lake ni kumaliza vita hivyo, Trump hapo kabla alikuwa ameonya kwamba makubaliano yoyote ya amani yanaweza kuhitaji Ukraine kutoa baadhi ya maeneo yake – pendekezo ambalo Zelensky amekuwa akilipinga kwa msimamo mkali.

Share: