Bw Khumalo, ambaye alitimuliwa hivi majuzi katika chama hicho, alisema Bw Zuma anashikilia nafasi hiyo kwa njia ya ulaghai
Tume ya uchaguzi ya Afrika Kusini Ilikuwa ikijibu barua ya mwanzilishi wa Chama cha MK Jabulani Khumalo, ambaye alitaka tume hiyo imwondoe Bw Zuma kama sura ya chama na kutoka kwenye orodha ya wanaotarajiwa kuwa wabunge.
Bw Khumalo, ambaye alitimuliwa hivi majuzi katika chama hicho, alisema Bw Zuma anashikilia nafasi hiyo kwa njia ya ulaghai kama kiongozi wa chama kipya.
Pia alimwandikia Bw Zuma, akimsimamisha kazi kwa tahadhari kwa kile alichosema ni "vitendo kadhaa vya utovu wa nidhamu".
Lakini katika taarifa ya Jumanne, Tume Huru ya Uchaguzi (IEC) ilisema haiingilii masuala ya ndani ya vyama vya kisiasa na ikathibitisha kwamba Bw Zuma alisalia kuwa kiongozi aliyesajiliwa wa chama cha MK.
"Tume hufanya kazi tu kwa maagizo ya kiongozi aliyesajiliwa wa chama," shirika la uchaguzi lilisema, na kuongeza kuwa Bw Zuma amesalia kuwa kiongozi wa chama cha MK tangu mwezi uliopita.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 82 amezuia majaribio ya kumzuia yeye, au chama chake kipya, kushiriki uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Mei.
Siku ya Ijumaa, Mahakama ya Kikatiba itasikiliza rufaa ya IEC kuhusu kupigwa marufuku kwa Bw Zuma kuwania kiti cha ubunge.
Mnamo Machi, tume ya uchaguzi ilijaribu kumzuia bila mafanikio kwa kudharau hukumu ya mahakama.